MWANAANGA wa Kijerumani Alexander Gerst
anatazamiwa kuwasili katika sayari ya dunia baada
ya kuwa katika Kituo cha Anga za juu cha kimataifa
kwa miezi sita. Gerst mwenye umri wa miaka 38
amekuwa akionyesha picha alizopiga na wanaanga
wenzake na mandhari ya dunia tokea alipowasili
katika kituo hicho cha Anga za juu cha Kimataifa ISS
hapo mwezi wa Mei.Gerst na wahandisi wenzake
Reid Wiseman wa Shirika la Utafiti wa Anga za juu la
Marekani NASA na Kamanda Maxim Suraev wa
Shirika la Anga la Urusi wanatarajiwa kutuwa nchini
Kazakhstan leo hii katika chombo chao cha anga za
juu cha Soyuz.
habari za sasa hivi kitaifa,kimataifa,makala,burudanina michezo
0 comments:
Post a Comment