habari za sasa hivi kitaifa,kimataifa,makala,burudanina michezo

Thursday, November 26, 2015

Posted by Benado kikoti | 8:20 PM | No comments




Papa Francis amesema ni jambo la aibu kama viongozi wa dunia hawatafikia muafaka juu ya namna ya kupambana joto duniani.

Akizungumza katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi, Kiongozi huyo wa Kanisa katoliki duniani amesema maslahi ya watu fulani hayapaswi kuruhusiwa kutawala ndani ya manufaa ya wote.

Kabla ya kuzungumzia hayo Papa Francis alikutana na viongozi wa dini ili kujadili umuhimu wa mazungumzo, na kuwa na misa za wazi kabla kukutana na umati wa maelfu ya waumini katika mji mkuu wa Kenya.

Katika ziara yake barani Afrika,kiongozi mkuu huyo wa kanisa katoliki anategemea kuelekea nchini Uganda leo na kuimalizia Jamhuri ya Afrika ya Kati novemba 30.

0 comments:

Post a Comment

Bookmark Us

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter