habari za sasa hivi kitaifa,kimataifa,makala,burudanina michezo

Monday, November 10, 2014

Posted by AMMY YEYOO | 9:20 AM | No comments
Mwanajeshi mmoja wa Israel amepigwa kisu katika kituo cha reli mjini Tel Aviv leo   na kwamba Mpalestina anayetuhumiwa kuhusika na uhalifu huo tayari ametiwa mbaroni.
 Msemaji wa polisi Micky Rosenfeld amesema mshambuliaji huyo alikuwa anatokea katika mji wa Ukingo wa magharibi wa Nablus na alikamatwa mara tu baada ya kutenda tendo hilo na kwamba hivi sasa anahojiwa.Msemaji katika hospitali ya Tel Aviv ambapo mwanajeshi huyo aliejuruhiwa anapatiwa mababu ameielezea hali yake kuwa mbaya.
Mvutano kati ya Waisrael na Wapalestina umezidi kuwa mkubwa katika wiki za hivi karibuni baada ya vita vya majira ya kiangazi yaliyopita katika Ukanda wa Gaza na kuzidi kwa mvutano wa eneo takatifu linalogombaniwa la Jerusalem. 
Kupigwa risasi na kuuwawa kwa Mu-israili mwenye asili ya Kiarabu hapo Jumamosi kumechochea upya mvutano huo baada ya mkanda wa video kuonyesha mtu huyo alikuwa akimuepuka  polisi wakati alipopigwa risasi na kuuwawa.

0 comments:

Post a Comment

Bookmark Us

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter