| Wamefariki watu takriban 5,000 Afrika Magharibi kutokana na Ebola |
Mgonjwa alikuwa mwanamume mganga wa kiisilamu aliyekuwa na umri wa miaka 50 na alikuwa ameingia nchini humo kutoka Guinea.
Alikuwa ametibiwa na muuguzi aliyefariki akiwa na umri wa miaka 25 mjini Bamako katika kliniki ya Pasteur ambayo kwa sasa imekfungwa na kuwekwa karantini.
Vifo hivi havijahusishwa na kifo cha mtoto mwenye umri wa miaka miwili aliyefariki kutokana na Ebola mwezi oKtoba.
Shirika la Afya Duniani limetangaza mlipuko huu wa Ebola kama janga la dunia.
| Aliyekuwa wa kwanza kufariki MALI kutokana na Ebola ni Mtoto mwenye umri wa miaka miwili |
Kesi hii ya Mali imeibuka siku moja baada ya shirika la Afya Duniani kuwatoa watu ishirini na tano karantini waliodhaniwa kumkribia msichana wa miaka miwili aliyefariki Oktoba .
Walikuwa miongoni mwa watu 100 waliokuwa karantini.
Kisa cha mtoto huyo kuugua na kufariki kutokana na Ebola kimewashangaza sana maafisa wakuu kwani inaarifiwa alisafiri kwa basi kutoka Guinea kuja Mali.
Takriban watu 5,000 wamefariki kutokana na Ebola katika mataifa ya Afrika Magharibi hasa nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone.
0 comments:
Post a Comment