habari za sasa hivi kitaifa,kimataifa,makala,burudanina michezo

Thursday, November 26, 2015

Posted by Benado kikoti | 8:27 PM | No comments



Bao la Dakika ya 78 la Harry Kane limewapeleka Tottenham Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya EUROPA LIGI huku wakiwa na Mechi 1 mkononi ya Kundi lao waliposhinda Ugenini 1-0 dhidi ya Qarabag Agdam FK ya Azerbaijan.
Kane alifunga Bao hilo kutokana na Kona ya Christian Eriksen huku Heung-Min Son na Dele Alli had hit the woodwork awakikosa Bao kwa Tottenham baada ya Mashuti yao kugonga Posti.
Image result for TOTTERNHAM VS QARABAG
VIKOSI:
Qarabag [Mfumo 4-2-1-3]: Sehic; Medvedev, Huseynov, Sadygov, Agolli; Garayev, Almeida; Quintana; Taghiyev, Poepon, Ismayilov
Akiba: Veliyev, Gurbanov, Yunuszada, Michel. Mammadov, Chumbinho, Armetertos.
Tottenham [Mfumo 4-2-3-1]: Lloris; Trippier, Alderweireld, Vertonghen, Davies; Dier, Mason; Alli, Eriksen, Son; Kane
Akiba: Vorm, Wimmer, Carroll, Townsend, Onomah, Winks, Njie.
EUROPA LIGI
**MECHIDEI 5 [Bado Mechi 1 kumaliza Makundi]
RATIBA/MATOKEO:
Alhamisi Novemba 26
FC Dinamo Minsk - Belarus 1 FC Viktoria Plzen - Czech Republic 0  
FC Rubin Kazan – Russia 2 FC Sion – Switzerland 0    
FK Krasnodar – Russia 1 BV Borussia Dortmund – Germany 0
SS Lazio – Italy 3 FC Dnipro Dnipropetrovsk – Ukraine 1     
AZ Alkmaar - Netherlands  1 FK Partizan – Serbia 2
Schalke 04 – Germany 1 Apoel Nicosia - Cyprus          0
AS Monaco FC – France 0  RSC Anderlecht – Belgium 2       
FC Basel 1893 – Switzerland 2 ACF Fiorentina – Italy 2        
Lokomotiv Moscow – Russia 2 Sporting CP – Portugal 4       
Besiktas – Turkey 2  Skenderbeu – Albania 0    
AC Sparta Prague - Czech Republic 1 Asteras Tripolis FC – Greece 0
Rosenborg BK – Norway 1 Saint Etienne – France 1  
Os Belenenses – Portugal 0 KKS Lech Poznan – Poland 0      
FC Augsburg – Germany 2 Athletic de Bilbao – Spain 3        
Qarabag Agdam FK – Azerbaijan 0 Tottenham Hotspur – England 1
23:05 Liverpool - England vs FC Girondins de Bordeaux - France    
23:05 Villarreal CF - Spain vs SK Rapid Wien - Austria
23:05 Olympique de Marseille – France vs FC Groningen - Netherlands     
23:05 Club Brugge KV – Belgium vs SSC Napoli - Italy
23:05 Celtic – Scotland vs Ajax Amsterdam - Netherlands    
23:05 Molde FK – Norway vs Fenerbahce - Turkey     
23:05 Sporting Braga – Portugal vs Slovan Liberec - Czech Republic         
23:05 PAOK FC – Greece vs FK Gilan Gabala - Azerbaijan     
23:05 Legia Warszawa – Poland vs FC Midtjylland - Denmark
MAKUNDI
Safari ya Fainali huko Basel, Uswisi:
Mechidei 1: 17 Septemba
Mechidei 2: 1 Oktoba
Mechidei 3: 22 Oktoba
Mechidei 4: 5 Novemba
Mechidei 5: 26 Novemba
Mechidei 6: 10 Desemba

KALENDA
Raundi ya Timu 32-Droo: 14 Desemba, Nyon
Raundi ya Timu 32-Mechi ya Kwanza: 18 Februari
Raundi ya Timu 32-Mechi ya Pili: 25 Februari
Raundi ya Timu 16-Droo: 26 Februari, Nyon
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Kwanza: 10 Machi
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Pili: 17 Machi
Robo Fainali-Droo: 18 Machi, Nyon
Robo Fainali-Mechi ya Kwanza: 7 Aprili
Robo Fainali-Mechi ya Pili: 14 Aprili
Nusu Fainali-Droo: 15 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Kwanza: 28 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Pili: 5 Mei
Fainali: 18 Mei, St. Jakob-Park, Basel, Uswisi
Posted by Benado kikoti | 8:20 PM | No comments




Papa Francis amesema ni jambo la aibu kama viongozi wa dunia hawatafikia muafaka juu ya namna ya kupambana joto duniani.

Akizungumza katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi, Kiongozi huyo wa Kanisa katoliki duniani amesema maslahi ya watu fulani hayapaswi kuruhusiwa kutawala ndani ya manufaa ya wote.

Kabla ya kuzungumzia hayo Papa Francis alikutana na viongozi wa dini ili kujadili umuhimu wa mazungumzo, na kuwa na misa za wazi kabla kukutana na umati wa maelfu ya waumini katika mji mkuu wa Kenya.

Katika ziara yake barani Afrika,kiongozi mkuu huyo wa kanisa katoliki anategemea kuelekea nchini Uganda leo na kuimalizia Jamhuri ya Afrika ya Kati novemba 30.

Tuesday, November 24, 2015

Posted by Benado kikoti | 8:14 PM | No comments

okcWestbrook alikuwa na pointi 31 na pasi 11 , akafunga  vikapu viwili muhimu katika sekunde 63 za mwisho, na Oklahoma City Thunder wakatoka nyuma kwa pointi nyingi  katika robo tatu na kwenda  kushinda ushindi mgumu wa 117-114  na kuvunja mwendelezo wa kushinda michezo sita mfululizo wa Dallas MavericksI.

Serge Ibaka alikuwa na pointi 16, rebounds tisa na na kupiga block muhimu kabisa ya sekunde za mwisho  kwa Oklahoma City . Thunder ilikuwa bila nyota wake aliye nje kutokana na majeraha,  Kevin Durant kwa mchezo wa sita mfululizo. Oklahoma City imeshuhudia rekodi ya  3-3 akiwa hayupo.

Wachezaji watano wengine wa  Oklahoma City walifunga katika tarakimu mbili yaani zaidi ya pointi 10, ikiwemo Serge  Ibaka , Dion Waitersi (14) , Anthony Morrow (14) , Enes Kanter (12) na Nick Collison (10).

Deron Williams aliiongoza  Dallas kwa pointi 20, huku pia akikosa mtupo muhimu zikiwa zimebaki sekunde 8.4. Wesley Matthews alimaliza na pointi 18 , wakati Pachulia alikuwa na pointi 12 na 10 rebounds.
Posted by Benado kikoti | 8:11 PM | No comments
Barca
Messi akicheza mchezo wake wa pili tangu aliporejea kutoka kwenye majeruhi ya muda mrefu ameisaidia timu ke kuibuka na ushindi wa magili 6-1 dhidi ya AS Roma kwenye mchezo wa kundi E wa michuano ya UEFA Champions ligi uliochezwa usiku wa Jumanne November 24 kwenye uwanja wa nyumbani wa Barcelona Nou Camp.

Akiwa katika kiwango cha hali ya juu Messi alifanikiwa kutupia kambani goli mbili kwenye ushindi wa sita huku akisaidia kupatikana kwa magoli mengine. Messi alicheza kwa dakika zote 90 za mchezo dhidi ya Roma.
Barca 1
Ghalika ya magoli ilianza kuishukia Roma mapema kipindi cha kwanza baada ya Luis Suarez kufunga goli la kuongoza dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza, dakika tatu baada Lionel Messi akaifungia Barcelona goli la pili kabla ya Suarez hajaongea bao la tatu dakika ya 44 na kuifanya Barcelona kwenda mapumziko ikiwa kifua mbele kwa mabao 3-0.

Mvua ya magoli ilizidi kuiandama Roma kipindi cha pili baada ya beki wa Barcelona Gerrard Pique kupachika bao la nne dakika ya 56 huku Messi akirejea tena nyavuni dakika ya 60 na Adriano akahitimisha ushindi kwa kufunga goli la sita dakika ya 77.

Barca 2
Nyota wa Brazil na Barcelona Neymar yeye aliosa penati 77 na kushindwa kufunga goli na kuwa mchezaji pekee ambaye hakufunga goli kwenye umoja wa washambuliaji wa Barca (mapacha watatu).
Mshambuliaji wa AS Roma Edin Dzeko aliifungia timu yake bao pekee kwenye kipigo hicho ilichokipata timu yake huku akipoteza mkwaju wa penati ilioupata timu yake dakika ya 82.
Posted by Benado kikoti | 8:07 PM | No comments
 
 Image result for muller
 Bayern Munich wamepata ushindi wao wa 4 katika hatua ya makundi ya Champions League maimu huu – lakini leo pia ilikuwa ni siku ya Thomas Muller kuandika rekodi mpya na kuwazidi Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Raul.

  Muller alifunga goli la 3 la Bayern katika ushindi wa 4-0 vs Olympiakos lakini pia ushindi wa leo pia ulikuwa ni wa 50 kwa kiungo mshambuliaji huyo wa kijerumani katika ligi ya mabingwa wa ulaya.

Muller ameweka rekodi ya kuwa mwanasoka mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kutimiza idadi ya mechi 50 za ushindi katika Champions League – ametimiza idadi hiyo akiwa na miaka 26 na siku 72.

Raul alitimza idadi hiyo akiwa na umri wa miaka 26 na siku 257 hivyo Muller ameivunja rekodi hiyo.



Wednesday, November 11, 2015

Posted by Benado kikoti | 10:34 AM | No comments
Wahamiaji
Wahamiaji wengi wamekuwa wakifa maji wakijaribu kufika Ulaya

 Image caption Wahamiaji wengi wamekuwa wakifa maji wakijaribu kufika Ulaya
Viongozi wa Muungano wa Ulaya wanatarajiwa kutoa mabilioni ya euro kwa mataifa ya Afrika kuyawezesha kusaidia kupunguza mzozo wa wahamiaji Ulaya.

Tume ya Muungano wa Ulaya imesema itatoa €1.8bn (£1.3bn) na inatarajia mataifa zaidi ya EU yaahidi pesa zaidi.

Lengo la ufadhili huo ni kusaidia kusuluhisha matatizo ya kiuchumi na kiusalama ambayo huwafanya watu kutoroka mataifa ya Afrika. Aidha, zitatumiwa kuyashawishi mataifa ya Afrika kuwapokea watu ambao wamenyimwa hifadhi Ulaya.

Ahadi hiyo inatarajiwa kutolewa kwenye mkutano mkuu kuhusu wahamiaji unaofanyika Malta, na ambao ulipangwa baada ya meli iliyobeba wahamiaji kuzama Libya mwezi Aprili. Watu 800 walifariki
Watu 150,000 wamevuka bahari ya Mediterranean kutoka Afrika mwaka huu, wengi wakitua Italia na Malta.

Hata hivyo, mtazamo wa EU umebadilika tangu Aprili na kuangazia zaidi wakimbizi wanaotoka mashariki na hasa Syria, ambao wanawasili kwanza Ugiriki na kuvuka hadi Uturuki kisha kuelekea kaskazini kupitia bataifa ya Balkan.

Zaidi ya viongozi 60 kutoka Afrika na Ulaya, akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, wanakutana Valletta, Malta kwa mkutano huo mkuu wa siku mbili kujadili uhamiaji.

Tume ya Muungano wa Ulaya itaweka pesa hizo €1.8bn kwenye "hazina maalum" kwa ajili ya Afrika na imehimiza mataifa wanachama kufikisha kiasi hicho cha pesa.

Hata hivyo, kuna shaka kuhusu iwapo mataifa hayo yatakubali wito huo.

Tuesday, November 10, 2015

Posted by Benado kikoti | 8:54 PM | No comments

  Rais wa Zanzibar Dokta Ali Mohammed Shein


Mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa visiwani Zanzibar yameendelea huku mkutano uliowaleta pamoja rais Ali Mohammed Shein na kiongozi wa upinzani Seif Sharif Hamad ukifanyika.

Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, mkutano huo wa faragha katika ikulu ya rais ulihudhuriwa na marais wa zamani Ali Hassan Mwinyi na Amani Abeid karume.

Ni mara ya kwanza kwa Dkt Shein ambaye anatoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Bw Seif wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye ni makamu wa rais wa kisiwa hicho kukutana tangu tume ya uchaguzi kufutilia mbali matokeo ya urais.

Kushirikishwa kwa marais hao wa zamani ni thibitisho kwamba kuna harakati za kisiasa zinazoendelea katika juhudi za kukabiliana na tatizo hilo ambalo limezua mgogoro wa kikatiba.

Wanachama wa jumuiya ya kimataifa pia wanadaiwa kushiriki katika kumaliza tatizo hilo.
Hakuna habari zilizotolewa kutoka pande zote mbili lakini duru za serikali zimethibitisha kwamba mazungumzo hayo yalifanyika kwa faragha.


 
Maalim Seif Hamad wa Zanzibar
Makamu wa rais wa pili Seif Ali Idd pia amedaiwa kuhudhuria mkutano huo kulingana na duru hizo.
Bw Mwinyi alikuwa rais wa Zanzibar kwa kipindi kifupi kabla ya kuteuliwa kuwania urais mwaka 1985 huku Karume akiliongoza eneo hilo kutoka mwaka 2000 hadi mwaka 2010.

Maafisa wa ikulu ya rais visiwani Zanzibar hawakuwa tayari kuzungumzia kuhusu yalioafikiwa katika mkutano huo.

Wale kutoka CUF hata hivyo wamesema kuwa majadiliano yalikuwa mazuri kwa maslahi ya raia wa muungano wa Tanzania.

Thursday, November 5, 2015

Posted by Benado kikoti | 10:43 AM | No comments


John Pombe Magufuli sasa ndiye rais mpya wa taifa la Tanzania baada ya kuapishwa rasmi kufuatia ushindi wake wa wingi wa kura katika uchaguzi mkuu uliopita.

Akiapishwa katika hafla iliohudhuriwa na viongozi mbalimbali,wakiwemo marais kutoka mataifa ya Afrika mashariki na kusini, Magufuli ameapa kutimiza ahadi zote alizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi.

Magufuli ambaye sasa ni rais wa awamu ya tano nchini Tanzania vilevile amewataka viongozi wa upinzani nchini humo kukubali kushindwa na kushirikiana naye katika juhudi zake za kuimarisha maisha ya taifa hilo.



Amesema kuwa licha ya kwamba alipata changomoto kubwa kutoka kwa upinzani alioupata amepata funzo kubwa kutoka kwao.

''Nashukuru wagombea wenzangu kwa kutupa changamoto,tumejifunza mengi kutoka kwao,lakini pia wajue kwamba uchaguzi umekwisha na rais ni John Pombe Magufuli'',alijigamba.


 
Awali aliyekuwa rais wa taifa hilo Jakaya Mrisho Kikwete aliwasili katika uwanja wa sherehe hiyo mbele ya umati mkubwa wa watu waliomkaribisha kwa vifijo na nderemo
.
Kikwete aliuzunguka uwanja huo akiwapungia mkono wa kwaheri raia hao waliojaa uwanja huo.
 Baadaye Bendera ya utawala wake ilishushwa huku rais mpya John Magufuli akiapishwa na makamu wake wa rais Samia Suluhu Hassan.

Bookmark Us

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter