Dar es Salaam.
Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni daktari feki amekamatwa katika Hospitali ya Muhimbili, kitengo cha Moi akiwa na vifaa mbalimbali vya kitabibu, ikiwamo majina ya dawa zinazotumika wakati na baada ya kutoa mimba.
Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni daktari feki amekamatwa katika Hospitali ya Muhimbili, kitengo cha Moi akiwa na vifaa mbalimbali vya kitabibu, ikiwamo majina ya dawa zinazotumika wakati na baada ya kutoa mimba.
Daktari huyo feki alikamatwa jana saa 3.00 asubuhi akiwa amevalia koti la kidaktari ndani ya majengo ya hospitali hiyo.
Kaimu Ofisa Uhusiano wa Moi, Frank Matua alisema
mtu huyo aliyetambulika kwa jina la Dismas John amedaiwa kuwatapeli
wagonjwa hospitalini hapo kwa kujifanya daktari anayeweza kuwasaidia kwa
haraka na kuwalipisha fedha.
Alisema kabla ya kukamatwa Dismas alikuwa katika
harakati za kuwatapeli wafanyakazi wa Moi kwa kutembeza karatasi ya
mchango akidai amefiwa na mkewe.
Matua alisema walipompekua walimkuta akiwa na
mipira ya mikono inayotumiwa na madaktari, karatasi yenye majina ya dawa
nyingi za kutolea mimba, kitabu cha mwongozo kitakachotumiwa na
madaktari wa wanawake na kitambulisho cha kupigia kura.
“Inaonekana amebobea katika masuala ya utaoji
mimba kwa vitu alivyokutwa navyo lazima awe anajihusisha na vitendo
hivyo,” alisema.
Alisema baada ya kukamatwa, daktari huyo feki
alipelekwa katika Kituo cha Polisi Selander Bridge kwa ajili ya hatua
zaidi za kisheria.
Gazeti hili lilimtafuta kwa njia ya simu, Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki kuzungumzia suala hilo, lakini
alijibu kupitia ujumbe mfupi kuwa yuko katika kikao.
Hospitali ya Muhimbili licha ya kuwa na utaratibu
wa kutumia vitambulisho kwa wafanyakazi wake, bado tatizo hili limekuwa
likijirudia mara kwa mara. Hili ni tukio la nne kutokea katika hospitali
hiyo.
0 comments:
Post a Comment