Serge Ibaka alikuwa na pointi 16, rebounds tisa na na kupiga block muhimu kabisa ya sekunde za mwisho kwa Oklahoma City . Thunder ilikuwa bila nyota wake aliye nje kutokana na majeraha, Kevin Durant kwa mchezo wa sita mfululizo. Oklahoma City imeshuhudia rekodi ya 3-3 akiwa hayupo.
Wachezaji watano wengine wa Oklahoma City walifunga katika tarakimu mbili yaani zaidi ya pointi 10, ikiwemo Serge Ibaka , Dion Waitersi (14) , Anthony Morrow (14) , Enes Kanter (12) na Nick Collison (10).
Deron Williams aliiongoza Dallas kwa pointi 20, huku pia akikosa mtupo muhimu zikiwa zimebaki sekunde 8.4. Wesley Matthews alimaliza na pointi 18 , wakati Pachulia alikuwa na pointi 12 na 10 rebounds.
0 comments:
Post a Comment