habari za sasa hivi kitaifa,kimataifa,makala,burudanina michezo

Tuesday, December 9, 2014

Posted by AMMY YEYOO | 5:53 AM | No comments
Dar es Salaam.

Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni daktari feki amekamatwa katika Hospitali ya Muhimbili, kitengo cha Moi akiwa na vifaa mbalimbali vya kitabibu, ikiwamo majina ya dawa zinazotumika wakati na baada ya kutoa mimba.
Daktari huyo feki alikamatwa jana saa 3.00 asubuhi akiwa amevalia koti la kidaktari ndani ya majengo ya hospitali hiyo.
Kaimu Ofisa Uhusiano wa Moi, Frank Matua alisema mtu huyo aliyetambulika kwa jina la Dismas John amedaiwa kuwatapeli wagonjwa hospitalini hapo kwa kujifanya daktari anayeweza kuwasaidia kwa haraka na kuwalipisha fedha.
Alisema kabla ya kukamatwa Dismas alikuwa katika harakati za kuwatapeli wafanyakazi wa Moi kwa kutembeza karatasi ya mchango akidai amefiwa na mkewe.
Matua alisema walipompekua walimkuta akiwa na mipira ya mikono inayotumiwa na madaktari, karatasi yenye majina ya dawa nyingi za kutolea mimba, kitabu cha mwongozo kitakachotumiwa na madaktari wa wanawake na kitambulisho cha kupigia kura.
“Inaonekana amebobea katika masuala ya utaoji mimba kwa vitu alivyokutwa navyo lazima awe anajihusisha na vitendo hivyo,” alisema.
Alisema baada ya kukamatwa, daktari huyo feki alipelekwa katika Kituo cha Polisi Selander Bridge kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Gazeti hili lilimtafuta kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki kuzungumzia suala hilo, lakini alijibu kupitia ujumbe mfupi kuwa yuko katika kikao.
Hospitali ya Muhimbili licha ya kuwa na utaratibu wa kutumia vitambulisho kwa wafanyakazi wake, bado tatizo hili limekuwa likijirudia mara kwa mara. Hili ni tukio la nne kutokea katika hospitali hiyo.

Monday, December 8, 2014

Posted by Unknown | 8:59 PM | No comments






Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Tanzania bara leo inaadhimisha miaka 53 toka ilipojipatia uhuru toka kwa Muingereza Desemba 9, mwaka 1961.
Maadhimisho haya ya 53 ni muhimu kwa Watanzania, kutokana na kwamba nchi ipo katika kipindi cha uchaguzi, ambapo Watanzania siku ya Jumapili Desemba 14, watapiga kura, katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji.

Uchaguzi huo ni muhimu, kutokana na viongozi katika ngazi hiyo kuwa karibu kabisa na jamii.
Tanzania pia inaadhimisha miaka 53 ya uhuru wake ikiwa katika harakati za uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Ni miaka 53 tangu Tanzania ijipatie uhuru wake, lakini hali za Watanzania wengi bado ni duni, kiuchumi na kijamii.
Posted by Unknown | 7:38 PM | No comments

Bi.Valerie Amos mkuu wa kitengo cha misaada wa umoja wa Mataifa
     

Mkuu wa kitengo cha misaada cha Umoja wa Mataifa Valerie Amos ,amesema kwamba hali ya sasa nchini Syria ni doa katika jamii ya kimataifa,ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mkakati mkubwa wa misaada ya kibinadamu kuwahi kutokea.

Bi Valie Amos amesema kwamba zaidi ya dola milioni kumi na sita zinahitajika kusaidia harakati za Umoja wa mataifa duniani kwa mwaka ujao,na nusu ya fedha hiyo inahitajika nchini Syria pekee.

Umoja huo umesema kwamba wa Syria wapatao milioni tatu wameikimbia nchi yao kufuatia mapigano yanayoendelea na kukimbilia nchi jirani na wengine milioni kumi na mbili wenye uhitaji wakiwa wametawanyika nchini humo.

Juma lililopita kitengo cha chakula cha umoja huo,kililazimika kupunguza kiwango cha misaada ya chakula kwa wakimbizi wa Syria kutokana na ukosefu wa misaada ya kibinadamu.

Inaarifiwa kwamba kiasi cha dola za kimarekani bilioni kumi na tatu kilichoombwa na umoja wa Mataifa kwa mwaka huu wa 2014 hawakupewa zote.

Bookmark Us

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter